other blog

Jumatano, 29 Julai 2015

Platin kuwania uongozi wa fifa by wasonga mrombo..


Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini anatarajiwa kutangaza azma yake ya kuwania urais wa FIFA baadaye wiki hii.BBC imebaini kwamba Platini baada ya kuungwa mkono na mashirikisho ya soka kutoka mabara manne atakuwa mgombea wakati uchaguzi wa shirikisho la soka duniani utakapofanyika februari 26 mwaka ujao.Platini mwenye umri wa miaka 60huenda akatangaza azma yake siku ya jumatano.Raia wa Uswizi Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 amekuwa akilisimamia shirikisho hilo tangu mwaka 1998.Anastaafu mwezi Februari kutokana na kashfa ya ufisadi katika shirikiso la FIFA.Na Platini anapigiwa upatu kumrithi.Anaungwa mkono na shirikisho lasoka barani Ulaya UEFA,shirikishola soka kusini mwa Marekani Conmebol,shirikisho la kaskazini,America ya kati na visiwa vya Carebean, Concacaf nalile la Asia AFC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni