other blog

Jumatano, 22 Julai 2015

Gereza la Guantanamo lakaribia kufungwa




Ikulu ya White house imesema kuwa
mipango ya kulifunga gereza la
Guantanamo Bay nchini Cuba imefikia
awamu za mwisho. Rais Barack
Obama anasemekana kupatia kipa
umbele suala la gereza hilo tangu
aingie madarakani mwaka wa 2009
lakini limekumbwa na vizuizi kadhaa.
Gereza hilo la Guantanamo, ambalo
limepewa jina la umaarufu kuwa Gitmo -
limekuwa likitumiwa na Marekani
kuwazuilia wapiganaji kutoka vita vya
Iraq na vya Afghanistan bila kufunguliwa
mashtaka yoyote. Rais Obama alitoa
agizo la kirais kufungwa kwa kituo hicho
mara moja katika siku yake ya kwanza.
Lakini baraza la Congress lilikataa
kuwahamisha wafungwa wa huko
kuwaleta nchini Marekani kutokana na
hofu za kiusalama.
Baadhi ya wadadisi wanaamini kuwa
Marekani ilifungua gereza hilo nje ya
ardhi ya Marekani ili wanajeshi wake
wapate fursa ya kutumia mbinu
zilizopigwa marufuku katika ardhi yao za
kuwahoji wafungwa.
Gereza hilo pia limekumbwa kwa miaka
mingi na madai ya ukiukajji wa haki za
binadamu, ambapo njia zilizotumika
kuwahoji wafungwa zimekashifiwa kuwa
ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
Aidha wafungwa wengi wamedai
kuteswa, kupigwa na hata kulazimishwa
kukiri baadhi ya mashtaka.
Wafungwa kadhaa maejaribu kujitoa uhai
kutokana na mateso wanayodai kupata
huko. Wengine wamechukua hatua kama
kususia kula kwa wiki kadhaa kama njia
ya kulalamika hali duni ya kibinadamu
katika gereza hilo.
Wengi tayari wamerejeshwa nchini mwao
japo kunao baadhi ambao wanaaminiwa
kuwa hatari zaidi na hivyo hawaja
achiliwa.
Msemaji mmoja wa ikulu ya white house
ameambia waandishi kuwa mipango ya
kuwasafirisha wafungwa hao kwa njia
salama imefikia awamu za mwisho na
itawasilishwa kwa baraza la Congress,
lakini hakutoa maelezo zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni