other blog

Jumanne, 28 Julai 2015

Wahamiaji ufaranza wakabiliwa vikali...


Kampuni wa usafiri inayofanya safari
zake kati ya Ufaransa na Uingereza ya
Eurotunnel imesema maelfu ya
wahamiaji wamekuwa wakijaribu
kuingia nchini Uingereza kupitia
usafiri huo.
Ripoti ya kampuni hiyo imebainisha kuwa
idadi ya majaribio ya wahamiaji kutaka
kuvuka mpaka kupitia usafiri aina hiyo ya
usafiri imeongezeka mno,kwani
wahamiaji hao watu hao wanajificha
kwenye magari ya mizigo,kupanda vizuizi
ilimradi tu waingine katika vyombo hivyo
vya usafiri na kuvuka.
Katika mkutano wa Mawaziri wa mambo
ya ndani wa Ufaransa na Uingereza
uliofanyika mjini London,mbinu za
pamoja kuweza kudhibiti wahamiaji hao
kuvuka zimejadiliwa na kuelezea hali
kuwa ni tatizo kubwa kwa sasa.
Wahamiaji hao kutoka nchi za Sudani na
Afghanstan waliopo bandari ya Calais
nchini ufaransa ya Calais ndiyo
waliobainika kutaka kuvuka kwenda
nchini Uingereza kwa mfumo huo, wengi
wa wahamiaji hao wanatoka nchini Sudan
na Afghanstan.
Mwaziri hao wa mambo ya ndani wa
Ufaransa na Uingereza wanasema
wamebaliana tutafanya kazi pamoja
kuwarejesha wahamiaji hawa ambao
wengi wao wanatoka Afrika Magharibi,na
kuwahakikishia watu kwamba safari za
aina hii haziwi lango kuu la wahamiaji
kuingia Uingereza.
Na tayari serikali ya Ufaransa imekwisha
anza kuweza jitihada za ziada kama idadi
zaidi ya askari,na uingereza itatoa kiasi
cha paundi million saba kuimarisha
ulinzi,japo kuwa Mbunge wa Bunge la
Ulaya Claude Moraes anasema haamini
kama hatua ya kuwarejesha wahamiaji
hao makwao kutasaidia kutatua tatizo
hilo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni