other blog

Jumanne, 28 Julai 2015

kakaribishwa UKAWA, amejiunga nao? Majibu ni haya kwa Mbatia…

“ Watanzania wanataka mabadiliko,
wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta
nje ” >> Hii ni moja ya sentensi ambazo
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Monduli, Edward Ngoyai Lowassa
aliziongea Arusha May 30 2015
alipotangaza nia ya Kugombea Urais
kupitia CCM.

CCM ilikuwa na Wagombea zaidi ya 40
ambao walitangaza nia na kuchukua fomu
za Kugombea Urais 2015 lakini baadae
Chama hicho kikampitisha Dk. John
Pombe Magufuli kugombea nafasi hiyo,
baada ya hapo kukawa na headlines
nyingi sana kuhusu ishu ya Edward
Lowassa na UKAWA.
Viongozi wa Umoja wa UKAWA
wamekutana Dar na mmoja wa Viongozi
hao, James Mbatia amesema
wamekubaliana kumkaribisha Mbunge
Edward Lowassa ndani ya UKAWA na
wako tayari kumpa nafasi na kushirikiana
nae.
‘ UKAWA tunahitaji viongozi wenye sifa,
uwezo na weledi katika kulinda
kuheshimu na kusimamia rasilimali za
Taifa… Tunamwalika Edward Lowassa
ajiunge na UKAWA na tuko tayari
kushirikiana nae kuhakikisha tunaing’oa
CCM madarakani kwenye Uchaguzi Mkuu
ujao.. Tunaamini ana uwezo wa
kuhamasisha umma kuikataa CCM na
udhalimu wake ‘ >> James Mbatia .
Zimeandikwa stori nyingi kuhusu Mbunge
huyo kujiunga CHADEMA, kingine
kilichoibua maswali mengi ni ishu ya
UKAWA kuchelewesha kumtaja Mgombea
wao wa Urais… hapa ziko picha mbili
zilizoenea Mitandaoni zikimwonesha
Mbunge Edward Lowassa pamoja na
Viongozi wa UKAWA, kuna chochote
kinafuatia?



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni