other blog

Jumapili, 2 Agosti 2015

Arsenal kupambana na Chels


Ligi kuu ya Uingereza inaanza tena siku ya jumapili wakati ambapo mabingwa wa ligi hiyo Chelsea wanakutana na washindi wa kombe la FA Arsenal katika kombe la Charity Shield itakayogaragazwa katika uwanja wa Wembley.Mechi hiyo inajiri siku 64 baada ya kumaliza ligi hiyo na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villakatika fainali ya FA.Pende zote mbili hazijafanya usajili mkubwa katika msimu huu ijapokuwa kipa Petr Cech ataanzishwa dhidi ya timu yake yazamani Chelsea.Chelsea vilevile inaweza kumuanzisha mchezaji wao mpyaRadamel Falcao.Falcao mwenye umri wa miaka 29alihudumu katika kilabu ya Manchester United msimu uliopita lakini hakuweza kutamba kwani aliweza kufunga mabao 4 katika mechi 29 alizocheza pekee.Siku ya jumapili itazikutanisha timu hizo mbili huku mkufunzi waArsenal akitarajia kuishinda timu inayofunzwa na Mourinho kwa mara ya kwanza kati ya mechi 13 walizocheza huku wakufunzi hao wawili tayari wakitofautiana.Mourinho alisema kwamba Arsenal imetumia fedha nyingi msimu huu ikilinganishwa na Chelsea katika kipindi cha miaka kadhaa iliopita ,huku Wenger akijibu kwamba hasikizi kile watu wanachosema ama kufikiri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni