other blog

Jumamosi, 22 Agosti 2015

‘Mpishi wa filamu za Bongo Movie aliyeweka kapuni’ shahada ya uhandisi Mtunzi na mwongozaji wa filamu maarufu za Bongo Movie, Daniel Leonard Manege ametangaza kuachia


tunzi na mwongozaji wa filamu maarufu
za Bongo Movie, Daniel Leonard Manege.
Dar es Salaam. Mtunzi na mwongozaji
wa filamu maarufu za Bongo Movie,
Daniel Leonard Manege ametangaza
kuachia filamu mpya akilezeza kuwa
atatumia mfumo tofauti wa masoko ili
kuhakikisha filamu hiyo iitwayo “Safari
ya Gwalu” inawafikia wananchi katika
ubora unaotakiwa.
Manege ambaye ameandika filamu
nyingi maarufu zinazosisimua
watazamaji nchini, alisema kuwa
atatumia taaluma na uzoefu alionao
wa miaka minne sokoni kuhakikisha
anaziba mianya yote ya uharibifu
dhidi ya kazi yake.
Mwongozaji huyo aliyehitimu Shahada
ya Uhandisi wa Viwanda na Utawala
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), alisema ametumia zaidi ya
Sh20 milioni kutayarisha filamu hiyo
mpya ambayo mwigizaji mkuu ni Gabo
Zigamba na kwamba inamzungumzia
kijana aliyekwama kimaisha ambaye
aliamua kurudi shule ya msingi ili
apate elimu.
“Nimeshaandika filamu nyingi
zilizofanya vizuri sokoni na kujitwalia
tuzo nyingi za filamu hasa kwenye
tamasha la Ziff kila mwaka. Lakini
Safari ya Gwalu’ ni filamu yangu ya
kwanza kuiandaa. Niliamua kumtumia
Gabo kwenye filamu hii kwa sababu
alifanya vizuri katika Filamu ya Bado
Natafuta. Hiyo pia niliiandika mimi.
Kwa mujibu wa muswada wa Filamu
ya Safari ya Gwalu, niliona Gabo
anafaa na amefanya ilivyotakiwa.”
alisema Manege.
Alisema mapenzi yake katika tasnia
hiyo yalimfanya afikirie ni namna
atakavyofanya ili kuibadilisha fani
hiyo, akieleza kwamba kwake hakuna
hasara kuacha taaluma aliyosomea na
kuingia katika uwanja wa filamu.
“Filamu yangu ya kwanza kuiandika na
ikaingia sokoni na kupendwa ni; “U Me
and Him”, ilikuwa chini ya Jacob
Steven (JB), iliigizwa pia na JB
mwenyewe, Kajala, Cloud 112,”
alisema.
Alisema akiwa na JB alitunga filamu
nyingi, ikiwemo; Bado Natafuta;
Shkamoo Mzee; Nipende Monalisa; Dj
Benny; Nakwenda kwa Mwanangu na
nyinginezo.
Manage alibainisha kuwa kwa sasa
ameashandika filamu zaidi 10 na zote
zipo sokoni, ambapo alifanya kazi na
waigizaji mbalimbali akiwamo kama
Dk Cheni, Steve Nyerere, Wema
Sepetu, Gabo, Shamsa Ford na
wengineo.
Hata hivyo alisema licha ya kukaa kwa
muda mrefu katika tasnia hiyo,
hajawahi kufikiria kuwa mwigizaji bali
anatamani abadili mfumo wa masoko
katika tasnia hiyo.
“Nilikuwa naota ndoto za kuja kuwa
mkombozi wa tasnia hii, nashukuru
zimeanza kutimia kwa kuandika
filamu zilizokubalika, kujenga mtandao
wa masoko na hata ubora filamu
zenyewe. Nilijua siwezi kuwa
mwigizaji ila kuikuza tasnia.
“Unajua tasnia ya filamu imekuwa
ikikosa waandishi na , hivyo
wasomi tunatakiwa kuunganisha
nguvu katika sekta ya sanaa nchini
kwa kuwa filamu ni sekta pekee
inayoingiza kiasi kikubwa cha fedha
maeneo mengi ulimwenguni pia ni
muhimu sasa tusifikirie kuajiriwa
muda wote,” alisema Manege.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni