other blog

Ijumaa, 21 Agosti 2015

Friday, August 21, 2015Christopher Mtikila, Chipaka na Malisa Waenguliwa Mbio za Urais.......NEC Yasema Hawajatimiza Masharti. Lowassa,Magufuli WAPETA!!!


Wanasiasa wakongwe nchini, Christopher Mtikila na John Lifa- Chipaka wametupwa nje ya kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kushindwa kutimiza vigezo vya kisheria.Mchungaji Mtikila anawakilisha Chama cha Democratic Party (DP) na Chipaka anawakilisha Tanzania Democratic Alliance (TADEA). Vyama vyote hivyo vilianzishwa mara tu Sheria ya Usajili wa Vyama vya Siasa,Na. 11 ya 1992, ilipopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.Kupitia sheria hiyo, ndiyo ilitolewa ruhusa ya kisheria ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania. Kabla ya sheria hiyo, masuala ya siasa yalikuwa si katika mambo ya Muungano.Pigo la kukosa kuteuliwa kugombea urais, pia lilimpataDk. Godfrey Malisa Kahangwaaliyewakilisha Chama cha Kijamii (CCK), chama kilichoanzishwa miaka michache iliyopita, baada ya uchaguzi mkuu wa 2010.Akitangaza matokeo ya maombi ya vyama hivyo vitatu jioni hii, Mwenyekiti waTume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema ombi la Mchungaji Mtikila limekataliwa kwa sababu ameshindwa kuwasilisha tamko la kiapo la Mahakama Kuu, ingawa yeye aliapa lakinimgombea mwenza wake ambaye hakutajwa jina, hakufika na hakuna kiapo chake.Jaji Lubuva ambaye alifikia ngazi ya jaji wa Mahakama yaRufaa Tanzania, amesema Dk.Kahangwa hakutimiza idadi ya watu wanaotakiwa katika udhamini na amekosa mgombea mwenza kutoka upande wa Zanzibar.Kwa Lifa-Chipaka, ilielezwa kwamba hakutimiza vigezo kwa vile alishindwa kuwasilisha orodha ya wadhamini kutoka Zanzibar. kisheria walitakiwa watu 200 wenye kadi za kupigia kura.Wakati Chipaka amekosa wadhamini Zanzibar, upande huohuo chama hicho kimesimamisha mgombea urais, ambaye ni Juma Ali Khatibu, Naibu Katibu Mkuu.Mchungaji Mtikila alilalamika mara tu alipotangaziwa uamuzi na Jaji Lubuva, kwamba alicheleweshwa kwa utaratibu tu wa ofisi ya Tume kwani alifika mapema na kuripoti ofisini kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima Kwemboy.Mtikila alidai kuwa hakufika na mgombea mwenza wake kwa wakati kwa kuwa amepata tatizo la kuumiwa mkewe na kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi na kuamua kuahirisha safari.“Tulijitahidi hata kumtumia tiketi ya ndege lakini hakuwahi hapa. Hili tatizo ni la asili ambalo mtu analifahamu linaweza kutokea wakati wowote. Lakini mimi nimewahi hapa na jaji alinikubalia kuapa na kushauri nije kukujulisha kuwa mkinipa muda kusubiri kidogo nitakamilisha na kurudia kwake niape na mgombea mwenza akiwa amewasili,” alisema Mtikila katika kilio ambacho hakikuzingatiwa na Tume.Jaji Lubuva alisema kwa wote walioshindwa kutimiza masharti, maana yake wamekosa kuteuliwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa kwa utaratibu ulioandaliwa, hakuna muda wa kuwasubiri kukamilisha taratibu.Vyama vilivyofuzu kuteuliwa wagombea wao ni pamoja na Chadema, Edward Lowassa (mgombea mwenza Juma Duni Haji) wanaowakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA); ACT-Wazalendo Anna Mghwira na mgombea mwenza Hamad Mussa Yussuf na Dk. John Magufuli (na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan) wa CCM.Kampeni za urais zinaanza rasmi kesho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni