other blog

Alhamisi, 6 Agosti 2015

Prof. Lipumba ajiuzulu uenyekiti CUF (slaa na lipumba wenye uchu wa madaraka waisaliti ukawa)..


Prof Lipumba: Nafsi imenisuta, naachia ngaziKwa ufupiTamko hilo la Prof. Lipumba linahitimisha siku mbili za minong’ono na tetesi zilizogubika medani ya kisiasa nchini kuwa kiongozi huyo anaondoka katika chama hicho hali iliyolazimu wananchama, wapenzi na mashabiki wa kiongozi huyo kufurika makao makuu ya chama hicho Buguruni Dar es Salaam jana ili kujua hatma ya kiongozi wao huyo.By Louis Kolumbia, Mwananchi DigitalDar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba leo ametangaza kujiuzulu uenyekiti ndani ya chamahicho.Tamko hilo la Prof. Lipumba linahitimisha siku mbili za minong’ono na tetesi zilizogubika medani ya kisiasa nchini kuwa kiongozi huyo anaondoka katika chama hicho hali iliyolazimu wananchama, wapenzi namashabiki wa kiongozi huyo kufurika makao makuu ya chama hicho Buguruni Dar es Salaam jana ili kujua hatma ya kiongozi wao huyo.Akizungumzia sababu za kujiuzulu kwake, Profesa Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambaoCUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.Amesema Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo. SWALI JE WANATAKA KUGOMBEA MPAKA KIFO CHAO??? KAMA HAWANA SERA WAPITE HIVI WATUACHIE LOWASA WETU..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni