other blog

Ijumaa, 14 Agosti 2015

Kiungo Mzimbabwe asaini Simba tuungane na mwanspoti wetu rizik malya.

Dar es Salaam.Kiwango kizuri kilichoonyeshwa na kiungo Mzimbabwe aliyekuwa kwenye majaribio, Justice Majabvi kimeifanya klabu ya Simba kumpa mkataba wa miaka miwili.Kiungo huyo amekuwa mchezaji wa tatu wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika kutua Tanzania msimu huu baada ya mshambuliaji Donald Ngoma nakiungo Thabani Kamasoko kutuaYanga wakitokea klabu ya Platinum.Majabvi aliwasili nchini wiki mbili zilizopita ikiwa ni sehemu ya mapendekezo ya kocha Muingereza wa Simba, Dylan Kerr ambaye aliwahi kuwa naye kwenye klabu ya Vicem Hai Phong inayoshiriki Ligi Kuu ya Vietnam.Akizungumza jijini jana, rais wa Simba, Evance Aveva alisema Majabvi amepewa mkataba huo baada ya benchi la ufundi la timu hiyo chini ya kocha huyo Mwingereza kujiridhisha na uwezo wake pamoja na kiwango alichokionyesha kwenye majaribio.“Tumemsainisha Majabvi mkataba wa miaka miwili jana (juzi) usiku baada ya kocha kujiridhisha na uwezo wake. Tumempa uhuru kocha kwenye masuala yote ya kitimu, hususansuala zima la usajili,” alisema Aveva.Katika hatua nyingine, klabu hiyo jana imekabidhi mipira minane kwa shule za msingi za Chang’ombe na Mikocheni za jijini Dar es Salaam yenye thamani ya Sh2.5 milioni ikiwa ni sehemu ya mradi wake wa kuongeza wanachama watoto wa klabu hiyo.Makabidhiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana mbele ya ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya EAG Group inayosimamia biashara za Simba, Imani Kajula, wawakilishiwa shule hizo, viongozi wa klabuhiyo na waandishi wa habari.Akizungumzia kwenye hafla hiyo, Aveva alisema mpango huo utakuwa endelevu, ukiwa nalengo la kuifanya klabu hiyo kuwa imara ndani na nje ya Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni