other blog

Jumamosi, 22 Agosti 2015

Kaseja atua Mbeya, Ivo asaka timu nje Wakati dirisha la usajili likifungwa jana usiku, kipa Juma Kaseja amesaini mkataba wa miezi sita


Kipa Juma Kaseja (kushoto) akikabidhiwa
jezi na kiongozi wa Mbeya City. Katikati ni
Tippo Athuman akishudia tukio hilo.
Dar/Mbeya. Wakati dirisha la usajili
likifungwa jana usiku, kipa Juma
Kaseja amesaini mkataba wa miezi sita
wa kuichezea Mbeya City, huku
mwenzake Ivo Mapunda akitangaza
kusaka timu nje ya nchi.
Makipa hao wa zamani wa Taifa Stars,
Kaseja na Ivo msimu uliopita hakuwa
mzuri kwao kutokana na kuingia katika
migogoro na klabu zao, Yanga na
Simba.
Kaseja alikaa nje ya soka kwa muda
mrefu kutokana na kuwa na mgogoro
na klabu yake ya zamani Yanga
uliohusisha masuala ya kimkataba.
Mgogoro huo ulipelekea Yanga
kumpeleka Kaseja katika Makahama ya
Kazi, Kitengo cha Usuluhishi hata
hivyo bado kesi hiyo inaendelea, lakini
haimzuii kipa huyo kujiunga na timu
yoyote ili kuokoa kipaji chake.
Hata hivyo, juzi usiku Kaseja alisaini
mkataba wa miezi sita kuitumikia
Mbeya City katika msimu huu wa Ligi
Kuu unaotarajia kuanza Septemba 12.
Msemaji wa Mbeya City, Dismas Ten
alisema kusajiliwa kwa kipa huyo ni
kutokana na mapendekezo ya kocha
Juma Mwambusi aliyeuambia uongozi
wao kuhusu ubora wa kipa huyo.
‘’Ni kweli tumenasa kipa mwenye
uzoefu wa hali ya juu nchini na
amesaini miezi sita kwa ajili ya
kuitumikia Mbeya City,’’ alisema.
Aliongeza kuwa Kaseja bado yupo Dar
es salaam na muda wowote atatua
jijini Mbeya kwa ajili ya kuungana na
wachezaji wenzake kwa ajili ya
maandalizi ya Ligi Kuu.
Alisema vipimo vyote vya kiafya kwa
mchezaji huyo vimekamilika na
kwamba japo Kaseja amesaini mkataba
mfupi, lakini wana imani ataitoa
Mbeya City kutoka hapa ilipo na
kuifikisha katika hatua fulani.
Kocha Mwambusi alisema ameamua
kumuweka Kaseja katika kikosi hicho
kutokana na ubora wa kazi
anayoonyesha akiwa langoni.
“Kaseja ni kipa aliyekuwa akimvutia
wakati akiwa na timu mbalimbali
ikiwamo Yanga aliyokuwa akitumikia
misimu ya hivi karibuni na kwamba
ubora huo sasa atauonyesha akiwa na
Mbeya City.”
Wakati Kaseja akijikita Mbeya City,
swahiba wake, Ivo Mapunda wa Simba
alisema atarudisha fedha za usajili za
klabu hiyo na kuendelea na jitihada
zake za kwenda kucheza soka la
kulipwa nje ya nchi.
Mapunda aliyeidakia Simba kwa
misimu miwili akitokea Gor Mahia ya
Kenya aliingia katika utata wa usajili
wake baada ya viongozi wake kudai
anadengua kusaini mkataba huku yeye
akipinga hilo na kudai kuwa hakuna
kitu kama hicho.
Uongozi wa Simba ulidai kuwa
umeamua kuachana na kipa huyo kwa
madai ni msumbufu na hataki kusaini
mkataba kwani kila walipomtaka
kufanya hivyo alionekana kama hataki
na wakati walishampa Sh 10 milioni
ingawa Ivo alisema kuwa yupo kila
siku na alikuwa anaumwa na viongozi
wanajua sasa anashangaa kuambiwa
hataki kusaini mkataba.
Kipa huyo aliliambia gazeti hili jana
kuwa soka la Tanzania lina mizengwe
na linahitaji uvumilivu mkubwa na
yote yaliyotokea kwake anamwachia
Mungu ana atarudisha fedha za usajili
alizochukua.
Alisema malengo yake ni kucheza soka
la kulipwa nje ya nchi ingawa hadi
jana kama kuna timu iliyokuwa
ikimuhitaji ilipewa ruksa ya kufanya
naye mazungumzo kabla ya dirisha la
usajili kufungwa jana usiku.
“Nitarudisha fedha zao za usajili,
ingawa kwa sasa malengo yangu ni
kucheza nje ya nchi, lakini sizizuii
klabu za hapa zinazonihitaji
kuzungumza na mimi ili kucheza kwa
muda mfupi wakati naangalia mipango
mingine ya kwenda nje.
Simba iliamua kuachana na Ivo baada
ya kumsajili kipa Vincent Angban
kutoka Ivory Coast , pia ilikuwa mbioni
kumsajili kipa mwingine wa JKU ya
Zanzibar, Abdulrahiman Mohammed,
lakini inao makipa wengine chipukizi
Manyika Peter jr na Dennis Richard.
-

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni