other blog

Jumatano, 26 Agosti 2015

NEC yaonya vyama vya siasa vitakavyokiuka ratiba za kampeni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa


Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Kailima Ramadhani
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vyote
vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi
Mkuu wa Oktoba 2015, kuhakikisha
vinafuata na kuheshimu ratiba ya
uchaguzi waliyojiwekea.
Katika taarifa kwa njia ya video
iliyotumwa kwa vyombo vya habari,
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Kailima Ramadhani
amesema kuwa vyama vyote vilishiriki
katika kuandaa ratiba hiyo na kuwa
viliiridhia hivyo hawana budi
kuhakikisha wanaifuata.
“Tulikaa na vyama, mimi sikuamua hii
ratiba, wao walipendekeza na
wakakubaliana na wakatoa ratiba hii,
cha kwanza kabisa vyama vya siasa
wazingatie waliyoyaweka humu,”
alisema Kailima.
Aliongeza kuwa utaratibu huo upo kwa
mujibu wa Sheria ya Maadili ya
Uchaguzi ya 2015 na kuwa wakikiuka,
sheria itawakamata.
“Kwenye maadili (Sheria ya Maadili ya
Uchaguzi 2015) kuna eneo ambalo
vyama vya siasa na wagombea
wanakubaliana kuzingatia muda wa
kuanza kampeni na muda wa kumaliza
kampeni,” alisema.
Aliongeza kwa chama au wanasiasa
watakaokiuka wataitwa kwenye kamati
ya maadili na kuhojiwa na
wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Agizo hilo la NEC linakuja siku chache
baada ya CCM kuzindua kampeni zao
siku ya Jumapili katika viwanja vya
Jangwani jijini Dar es Salaam ambapo
shughuli hiyo ya uzinduzi ilihitimishwa
majira ya saa 12.34 jioni, ikiwa ni nusu
saa zaidi ya muda unaotakiwa
kisheria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni