other blog

Jumatano, 26 Agosti 2015

Na katika mchezo eaglefm..Samata, Ngassa, Uhuru wachemsha Haikuwa wiki nzuri kwa washambuliaji kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samata, Mrisho Ngassa na Uhuru




Mbwana Samata
Dar es Salaam. Haikuwa wiki nzuri
kwa washambuliaji kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Samata, Mrisho
Ngassa na Uhuru Selemani baada ya
klabu zao kupoteza katika michezo
yao.
Samata alishindwa kuisaidia TP
Mazembe kukwepa kipigo cha bao 1-0
kutoka kwa Al Hilal mchezo
uliofanyika Omdurman wa kusaka
kufuzu kwa nusu fainali ya Ligi ya
Mabingwa.
Kwa matokeo hayo Hilal inaongoza
Kundi A, ikiwa na pointi nane sawa na
Mazembe wakitofautiana mabao.
Wakati Samata akipata kipigo hicho
Ngassa alikuwa benchi kuishudia timu
yake ya Free States Stars ikipokea
kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa
mabingwa wa Ligi Kuu Afrika Kusini,
Kaizer Chiefs.
Katika mchezo wake wa kwanza na
Free State Stars, Ngassa alicheza
dakika 64 na kupata kadi ya njano
wakati timu yake ilipofunga bao 1-0 na
Mpumalanga Black Aces.
Hiyo ni mechi ya pili mfululizo kwa
Free States kupoteza tangu kuanza
kwa Ligi Kuu Afrika Kusini na sasa
inashika mkia kati ligi hiyo yenye timu
16.
Naye Uhuru Selemani hakucheza
wakati timu yake ya Jomo Cosmos
ilipolazimishwa sare 0-0 na Golden
Arrows katika mchezo wa Ligi Kuu
Afrika Kusini.
Hata hivyo, winga huyo wa zamani wa
Simba, Uhuru tangu asajiliwe Cosmos
bado hajaanza kuicheza timu hiyo
katika michezo ya Ligi Kuu.
-

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni