other blog

Jumapili, 2 Agosti 2015

NAFASI ZA KAZI TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI TAR 14 AGOSTI 2015

Jitihada za Serikali katika kupambana
na uhalifu wa mitandao imeungwa
mkono kutokana na baadhi ya vyuo
kuanzisha mitalaa yenye somo la ulinzi
wa mitandao.
Moja ya jitihada za serikali katika
kukabiliana na changamoto hiyo ni
kupeleka muswada wa sheria ya
uhalifu wa mtandao ya mwaka 2015
katika mkutano wa 19 wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambao ulipitishwa na Bunge hilo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknologia, Profesa Makame Mbarawa
anasema, kukua kwa kasi kwa
matumizi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (Tehama) kumeleta
mafanikio kwa kuongezeka kwa
biashara zinazotumia huduma za
mawasiliano, fedha na matumizi ya
mitandao.
Anaeleza kuwa hayo ni mapinduzi ya
maendeleo kwa kutumia teknolojia
lakini kwa upande mwingine yameleta
changamoto nyingi katika jamii
ikiwamo kuibuka kwa uhalifu na
kuibua makosa mapya ya jinai.
Makosa hayo, anasema yanajumuisha
uhalifu wa mitandao ambapo simu za
mkononi, kompyuta au mifumo ya
kompyuta hutumika kama nyenzo za
kutenda uhalifu huo.
Mifano ya makosa hayo ni pamoja na
wizi wa fedha kwa njia ya mtandao,
ugaidi, maudhui potofu
yanayosababisha mmomonyoko wa
maadili, uharibifu wa miundombinu
muhimu ya Taifa ikiwamo mkongo wa
Taifa wa Mawasiliano.
Mtaalamu wa Ulinzi wa Mitandao,
Ezekiel Mpanzo anasema tatizo la wizi
wa mitandao limekuwa kubwa na
kusababisha hasara kwa benki pamoja
na wananchi.
Mpanzo ambaye pia ni Mkuu wa Chuo
cha Teknolojia na Uongozi cha
Kilimanjaro, anasema kwa upande wa
vyuo vilivyopo chini ya Baraza la Taifa
la Elimu ya Ufundi (Nacte) pamoja na
vyuo vikuu wamegundua tatizo hilo na
wamejaribu kutengeneza mtalaa
ambao una somo la kuzuia wizi huo.
“Tumetengeneza mtalaa mzuri na
kuingiza somo la ulinzi wa mtandao.
Tumeuandaa sisi wenyewe na
kuupeleka Nacte na wameupitisha,
kwa hiyo tunaamini kwamba utasaidia
Taifa kupunguza tatizo hilo,” anasema
Mpanzo.
Anasema njia nyingine ya kuzuia tatizo
hilo ni wataalamu wa hapa nchini
kujiunga na vyama vya kuzuia uhalifu
wa mitandao duniani. “Wataalamu wa
hapa nchini, wakijiunga na vyama
hivyo, vikiwamo Ethical Hacking na
Sisco, itasaidia kubadilishana uzoefu
kuhusu mbinu wanazotumia wahalifu
duniani kote kutokana na mabadiliko
ya sayansi na teknologia,” anabainisha
Mpanzo.
Lengo lao, anasema ni nchi kuwa na
wataalamu wengi watakaosaidiana na
Serikali pamoja na taasisi mbalimbali,
kukabili tatizo la wizi kwa kutumia
mitandao.
Anasemakatika mwaka 2010 na robo
ya mwaka 2013 Tanzania ilipoteza
Sh9.8 bilioni kutokana na wizi huo
ambao ulifanywa katika mashine za
kutolea fedha maarufu kama ATM.
Hivi karibuni, Jijini Arusha ulifanyika
mkutano wa kujadili mbinu za kuzuia
wizi kwa kutumia mitandao katika
nchi za Afrika Mashariki ambapo
ilitolewa ripoti kuhusiana na vitendo
hivyo.
Akifungua mkutano huo, Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira
Silima anabainisha kuwa hapa nchini
kuna kesi zaidi ya 300 za uhalifu wa
mitandao ambazo zinachunguzwa na
baadhi ziko kwenye hatua ya
kufikishwa mahakamani.
Katika mkutano huo pia ikabainika
kuwa wizi huo umekuwa ukifanyika
kirahisi kutokana na nchi za Afrika
Mashariki kutokuwa na wataalamu wa
kutosha katika kukabili vitendo hivyo
haramu.
Wadau wengi wa mitandao kwenye
mkutano huo wanaweka wazi kuwa
kuna umuhimu wa kubadilishana
uzoefu kwa wataalam.
ADVERTISEMENT
Hii inatokana na ripoti iliyotolewa na
Kampuni ya Kaspersky lab ambayo
ilibainisha kuwa genge la wahalifu wa
mtandao lilifanikiwa kuiba mamilioni
ya Dola za Marekani kutoka kwenye
akaunti za wateja wa benki 1,000
katika mataifa 30 kati ya mwaka 2014
na 2015.
Wizi huo unaonekana ulianza mwaka
2013 na bado unaendelea kwenye
benki mbalimbali, huku kukiwa na
mbinu finyu katika kuukabili.
Ripoti hiyo ilitoa mfano wa mbinu za
genge la Carbanak, linatumia mbinu ya
kuambukiza virusi kwenye mashine na
kompyuta za benki ikiwamo kamera za
CCTV ili kunakili kila kitu
kinachoandikwa kwenye komputa.
Ripoti hiyo inaelezea mbinu mpya za
wahalifu mtandao wanazotumia
kudukua nambari za akaunti za wateja
za siri kabla ya kuingia na kuiba fedha.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, benki
katika mataifa 30 yakiwamo, Russia,
Marekani, Ujerumani, China, Ukraine
na Kanada yameathirika kwa asilimia
kubwa.
Kaspersky imesema kuwa wizi huo
ulianza mwaka wa 2013 na bado
unaendelea hata leo kwani hivyo benki
nyingi zinapaswa kuwa makini kwa
sababu bado uhalifu huo unaendelea.
Taarifa inaeleza kwamba genge la
wahalifu mtandao limefanikiwa kuiba
mamilioni ya Dola za Marekani kutoka
kwenye akaunti za wateja wa benki
100 katika mataifa 30 kati ya mwaka
2014 na 2015.
Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuli
zake nchini Urusi, Ukraine na Uchina.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo benki
katika mataifa 30, zikiwamo za Russia,
Marekani, Ujerumani, China, Ukraine
na Canada.
Uchunguzi mbalimbali wa kimataifa
unaonyesha kuwa wezi wamekuwa
werevu kiasi kwamba, huweza
kutumia teknolojia kupata taarifa za
siri za watumiaji wa kompyuta
zilizounganishwa kwenye mitandao.
Wanatumia programu mbalimbali
zinazoitwa virusi vya kompyuta kupata
taarifa hizo. Virusi hao ni kama vile
trojans, worms, viruses, hacktools,
rootkits na hadware.
“Siku hizi kuna uhusiano wa kampuni
hasa kati ya maharamia wa njia za
mitandao na kampuni au vikundi
vinavyojihusisha na jinai. Hawa ndio
wanaojihusisha na jinai na ndio mara
nyingi wanakuwa ni chanzo cha
kuwezesha kusambaza mafanikio ya
wizi kwa njia ya mtandao,” anasema
Daniel Kamau kutoka kampuni ya
inayojihusisha na utengenezaji wa
kompyuta pamoja na programu zake
ya Microsoft.
Baadhi ya mitandao inayoibuka na
kulaghai kwa kuwataka wananchi,
kutoa taarifa zao muhimu za kibenki,
jambo ambalo linahatarisha usalama
wa fedha zao zinazohifadhiwa na benki
hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk
Charles Kimei anasema kuwa
kumeibuka mchezo kwa baadhi ya
mitandao ya kijamii, ikijaribu
kuwalaghai wateja kwa kuwaomba
taarifa za akaunti zao ili kufanya
uhalifu.
Alisisitiza wananchi wanatakiwa kuwa
makini na kundi hilo, wasikubali
kudanganyika kwa kutoa taarifa
zinazohusiana na nyaraka nyeti za
benki zao na kusisitiza kuwa ni
marufuku kutoa taarifa hizo hata kwa
wafanyakazi wa benki.
Kauli ya Kimei inawiana na tamko la
mitandao ya simu linalowahadharisha
wateja wao kutotoa taarifa zao, hasa
namba ya siri za akaunti zao za fedha,
hata kama wanaozitaka
watajitambulisha ni wafanyakazi wa
mitandao husika.
Hali hii inaashiria kuwa wahalifu
wanatumia teknolojia ili kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu. Hii
inaashiria wazi kwamba Tanzania nayo
inapaswa kuweka mkakati wa hali ya
juu wa kuwa na wataalamu wa kutosha
ili kukabiliana na tatizo hilo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni