other blog

Jumatatu, 17 Agosti 2015

Wema sepetu rasmi sasa afunguliwa kushiriki miss tanzania


Dar es Salaam.Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limemfungulia mwandaaji wa shindano la urembo la Miss Tanzania, Lino International Agency baada ya kuomba radhi na kufanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza na kutekeleza masharti aliyopewa.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema LINO International Agency imepewa kibali cha muda kisichozidi miezi minne kwa ajili ya maandalizi ili kukamilisha usajili wa mawakalakatika ngazi husika.Mngereza amesema kuwa mapungufu yaliyobainishwa ni pamoja na kutofuata sheria,kanuni za uendeshaji matukio yasanaa nchini ,kutokuwakilisha nyaraka mbalimbali za shindanolake na mikataba ya washirki,kutumia mawakala ambao hawajasajiliwa na kupewa vibali na Baraza la sanaa la Taifa.Amesema miongoni mwa mapungufu yaliyofanyiwa kazi na Kampuni ya Lino ni mchakatowa kusajili mawakala na kufanyia marekebisho kanuni nataratibu za uendeshaji wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni