other blog

Jumanne, 4 Agosti 2015

Dr Dre kutoa albamu mpya ya muziki


Kwa miaka 15 mashabiki wa msanii Dr Dre wamekuwa wakingojea kwa hamu tangazo hilo muhimu.Na sasa hatimaye mwanamuziki huyo alitangaza wikendi hii katika kipindi cha rappa huyo kwamba albamu yake mpya itakuwa tayari ifikiapo Agosti tarehe 7.Lakini tulidhani kwamba mwanamuziki huyo ambaye pia nimtunzi alikuwa anaiandaa ile albamu yake kwa jina Detox.Lakini alisema kwamba albamu ya Detox haikuwa nzuri.''Sidhani kama nilifanya kazi nzurina siwezi kuwafanyia mashabiki wangu hivyo na vilevile sikuweza kujifanyia hivyo'',alisema.Akizungumza katika kipidi chake cha beat One ,amesema kuwa albamu hiyo mpya kwa jina The Pharmacy ilishawishiwa sana na rappa wa miaka mingi NWA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni