other blog

Jumatano, 26 Agosti 2015

Majambazi yauawa Mwanza Polisi mkoani hapa wamefanikiwa kuwauwa majambazi wawili baada ya kutupiana nao risasi kwa zaidi


Kamanda wa Polisi Mwanza, Charles
Mkumbo
Mwanza. Polisi mkoani hapa
wamefanikiwa kuwauwa majambazi
wawili baada ya kutupiana nao risasi
kwa zaidi ya dakika 10.
Majambazi hao ambao walikuwa
wanne wanadaiwa kutaka kufanya
uhalifu kwenye Kisiwa cha
Chembaya kilichopo katika Ziwa
Victoria juzi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
Mwanza, Charles Mkumbo majambazi
hao walikuwa wanatumia usafiri wa
pikipiki na kwamba walianza
kutupiana risasi na polisi baada ya
kubaini kuwa wanafuatiliwa na askari
waliopata taarifa dhidi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo, Kamanda amesema polisi walipata
taarifa saa 8:00 mchana juzi kutoka
kwa raia wema kwamba kuna kikundi
cha majambazi kinajiaanda kufanya
uhalifu Ziwa Victoria.
“Baada ya Polisi kupata taarifa hizo
walijipanga na kuweka mtego kwenye
eneo la mwalo wa Kisaka uliyopo
katika Kata ya Ilemela,” Kamanda
Mkumbo amesema na kuongeza:
Kwa mujibu wa jeshi hilo, silaha moja
aina ya Shotgun iliyofutwa namba na
kukatwa kitako na mtutu wake
zimepatikana baada ya majambazi hao
kupekuliwa walikutwa na riasi tano.
Kamanda Mkumbo amesema miili ya
majambazi hao imehifadhiwa katika
hospitali ya Rufaa Bugando, jijini
Mwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni