other blog

Jumatatu, 24 Agosti 2015

Pingamizi dhidi ya Profesa Maghembe latupwa Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mwanga ametupilia mbali pingamizi zilizowekwa na mgombea ubunge


Waziri wa Maji ambae pia ni Mbunge wa
Mwanga ,Profesa Jumanne Maghembe.
Mwanga . Msimamizi wa uchaguzi wa
Jimbo la Mwanga ametupilia mbali
pingamizi zilizowekwa na mgombea
ubunge kwa tiketi ya Chadema, Henry
Kileo dhidi ya wagombea wenzake
wawili.
Kileo aliweka pingamizi dhidi ya
Waziri wa Maji na mbunge
anayemaliza muda wake, Profesa
Jumanne Maghembe (CCM) na
Mgombea wa NCCR-Mageuzi,
Youngsaviour Msuya ambaye ni
wakili kitaaluma.
Kwa mujibu wa Kileo, wagombea hao
hawakuwa wamewasilisha tamko
rasmi la kisheria lililotolewa mbele ya
hakimu mkazi wa Wilaya ya Mwanga
na pia, hawakuwa wamedhaminiwa na
vyama vyao.
Kileo alidai mihuri iliyogongwa katika
fomu zao ni ya katibu wa wilaya
badala ya ofisi ya wilaya. Pia, alidai
kuwa picha ya Profesa Maghembe
haikupigwa ndani ya miezi mitatu.
Hata hivyo, msimamizi wa uchaguzi wa
jimbo hilo, Jamhuri William ametupilia
mbali sababu hizo akidai kuwa
kumbukumbu alizonazo ofisini kwake
wagombea hao wamedhaminiwa na
vyama vyao.
Alisema hatua ya Msuya kutoa tamko
mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya
ya Moshi haimuondolei sifa ya
kuteuliwa mgombea na pia, haoni
tatizo kwa Profesa Maghembe kula
kiapa Mahakama ya Mwanzo. “Masuala
yanayohusu mihuri ya chama
inategemea na muundo wa uongozi na
utendaji katika chama husika. Hakuna
kosa kwa katibu wa wilaya kugonga
muhuri wake,” alisema msimamizi
huyo.
William alifafanua kuwa suala la umri
wa picha ya Profesa Maghembe halina
uthibitisho na kwamba, malipo ya risiti
ya tamko rasmi siyo mojawapo ya
sharti la uteuzi wa mgombea ubunge.
Baada ya kutupwa kwa pingamizi lake,
Kileo aliliambia gazeti hili jana kuwa
atakata rufaa kwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) akipinga uamuzi huo
wa msimamizi kuwa haukutenda haki.
Kileo alisema mathalani katika
uchaguzi wa Serikali za Mitaa
uliofanyika mwaka jana, baadhi ya
wagombea wa Chadema walienguliwa
baada ya fomu zao kugongwa muhuri
na katibu wa wilaya.
-

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni