other blog

Jumatano, 26 Agosti 2015

LASTECK ALFRED 0 Recomendar DESKTOP VIEW BACK TO TOP Pluijm: Yondani, Cannavaro igeni Kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amewataka mabeki Ligi Kuu wakiwamo wa klabu yake, Kelvin Yondani


Kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm.
Dar es Salaam. Kocha mkuu wa Yanga,
Hans Pluijm amewataka mabeki Ligi
Kuu wakiwamo wa klabu yake, Kelvin
Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’
waige aina ya ukabaji wa beki wa
Azam, Pascal Wawa.
Alisema ukabaji wa nguvu na wa
kujiamini wa beki huyo raia wa
Ivory Coast ndiyo unaotakiwa kwa
sasa kwenye soka.
Alisema, “ Wawa (Pascal) ni beki
mahiri na anayetakiwa kuigwa na
mabeki wengine Ligi Kuu, lakini pia na
mabeki wangu Nadir Haroub
‘Cannavaro’ na Yondani (Kelvin) kwa
kuwa beki huyo anakaba kwa nguvu
wakati inapoitajika huku akijiamini.
“Wawa ana nguvu anazitumia nguvu
zake akijiamini na kujua wazi kuwa
anafanya kitu sahihi. Ukabaji wake
unafuata sheria za soka na hata
anavyofanya hivyo na wachezaji
kumlaumu basi ni wazi kuwa
wachezaji hawatambui kuwa anafanya
kazi yake inavyotakiwa.
“ Kizuri anachofanya ni kujiamini na
kujua sheria za soka, pia anatumia
nguvu akijua kuwa hajakosea wala
hatadhibiwa kwa kuwa anafanya kitu
sahihi na kwa muda mwafaka,”
alieleza kocha huyo.
Alisema kuwa ukabaji wa Wawa una
utofauti mkubwa na ule unaofanywa
na mabeki wengine Tanzania.
“Wawa anakaba kwa nguvu kwa
malengo na kujiamini, lakini mabeki
wengi ambao nimekuwa nikiona hapa
wanakaba kwa nguvu bila ya lengo la
kuisaidia timu kimpira zaidi
wanawaumiza wenzao, pia wanakaba
kwa nguvu bila kujiamini na chote
wanachokuwa wanafanya wanaona
kama vile wanakosea na mara nyingi
huwa wanajikuta wakipatwa na hofu
wanapokuwa wakikaba huku waamuzi
wakiwafuatilia kwa umakini,” alieleza.
-

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni