other blog

Jumapili, 2 Agosti 2015

Mtikila achukua fomu ya urais kwa shingo upande Wakati Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Christopher Mtikila akigoma kusaini fomu za


Mwenyekiti wa Democratic Party (DP),
Mchungaji Christopher Mtikila akisaini
nyaraka za Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(Nec) za kuthibitisha kupokea fomu za
kugombea Urais zilizokabidhiwa na Ofisa
Mwandamizi wa Tume hiyo George
Kashura jijini Dar es Salaam jana. Picha na
Said Khamis
ADVERTISEMENT
Dar es Salaam. Wakati Mwenyekiti wa
Chama cha Democratic Party (DP),
Christopher Mtikila akigoma kusaini
fomu za kugombea urais akitaka
ufafanuzi wa mgombea binafsi,
Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa
amekwama kwenye lifti za jengo
lililopo katika Ofisi za Tume ya
Uchaguzi (NEC) kutokana na kukatika
umeme.
Mchungaji Mtikila ambaye
aliambatana na mgombea mwenza
Juma Metu Juma, alitaka ufafanuzi wa
kutokuruhusiwa kuwania urais akiwa
mgombea binafsi wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wakati
Mahakama ya Haki za Binadamu ya
Afrika (AfCHPR) imeruhusu.
“Siondoki hapa na wala sitaweza
kuchukua hizi fomu hadi mniambie ni
wapi nitapata jibu la tume la kukiuka
maagizo ya mahakama ya Afrika.
“Waandishi embu subirini kwanza
mkurugenzi wa uchaguzi aje hapa ilia
atoe ufafanuzi na nyie msikilize
mkaandike ukweli kwa sababu hii siyo
haki ni sawa na kudharau mahakama,”
alisema.
Baada ya kuzozana na maofisa
waliokuwa wakimkabidhi fomu hizo,
walilazimika kumuita mkurugenzi wa
uchaguzi Kailima Ramadhani, ambaye
alimwambia kwamba sheria
hairuhusu.
“Sisi tunafuata sheria mwenyekiti
kama hicho kipengele kingekuwapo
tungekuruhusu uchukue fomu hizo,
lakini hapa tunabanwa na sheria
tunaruhusu kutoa fomu kwa watu
wanaotoka kwenye vyama vyao,”
alisema Ramadhani
Alisema ni vizuri Mtikila angefuatilia
kwa makini suala hilo ili sheria
ipitishwe kwani NEC wanachokifanya
ni kufuata sheria zilizopo tu na si
vinginevyo.
Baada ya kumaliza maongezi Mtikila
aliamua kuweka sahihi na kuchukua
fomu hizo kwa shingo upande huku
akisema atakiwakilisha vyema chama
chake hicho.
Juni 13,2013 Mtikila alishinda kesi
aliyofungua AfCHPR, mjini Arusha
akidai Tanzania inakiuka demokrasia
inapozuia wagombea binafsi.
Mchungaji Mtikila, ambaye ana
historia ndefu ya kukwaruzana na
Serikali ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), alifungua shauri mahakama ya
Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada
zake za kupindua mabadiliko ya
kikatiba yaliyofuta ugombea binafsi
kugonga mwamba kwenye mahakama
za kitaifa.
Dovutwa
Mwenyekiti wa UPDP Fahmi Dovutwa
alikwamba kwenye lifti kwa dakika
kumi baada ya jana kuchukua fomu za
kuwania urais.
Dovutwa ambaye alikuwa wa kwanza
kufika kuchukua fomu saa tatu
asubuhi, akiwa ameambatana na
mgombea mwenza, alisema kwamba
kukwama kwake kwenye lifti ni
hujuma iliyofanywa na baadhi ya
wagombea wenzake wa urais.
Wakati huohuo; Mgombea urais kwa
tiketi ya TLP Maxmilian Lyimo,
ambaye hakuwa na mgombea mwenza
alikuwa wa pili kufika katika ofisi hizo
kwa ajili ya kuchukua fomu.
Mgombea huyo alifika saa 5:33
asubuhi baada ya kuchukua fomu
alisema kuwa upepo wa Uchaguzi
Mkuu unaovuma mwaka huu,
haukuwahi kuvuma wakati mwingine
wowote, hivyo inaashiria kuwa nchi
itapata kiongozi asiyetarajiwa na
wengi.
“TLP ni chama kisichochafua amani
tangu kuasisiwa kwake, hivyo
wananchi waangalie amani ya nchi
kwani ni bora kuliko kitu
kingine,”alisema na kuongeza:
“TLP bado kuna nafasi za uongozi
kuanzia kata hadi za ubunge,
wanaoshindwa huko waliko
tunawakaribisha kwa ajili ya kuja
kugombea nafasi hizo.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni