other blog

Jumatano, 26 Agosti 2015

Simba waleta msenegal mwingine... 0 Recomendar DESKTOP VIEW BACK TO TOP Niang mmh! Mwingine aja Wakati Papa Niang akishindwa kuonyesha makali yake Simba ikilazimishwa suluhu na Mwadui, leo




Mshambuliaji mpya wa Simba, Papa Niang
Dar es Salaam. Wakati Papa Niang
akishindwa kuonyesha makali yake
Simba ikilazimishwa suluhu na
Mwadui, leo itampokea mshambuliaji
mwingine kutoka Senegal, Pape
Abdoulaye N’Daw anayetarajiwa kutua
jijini Dar es Salaam akitokea Dakar.
Macho na masikio ya mashabiki wa
Simba jana yalikuwa kwa Niang
aliyecheza mechi yake ya kwanza
Tanzania, lakini alishindwa kukata kiu
ya mashabiki wake waliojitokeza
kwenye Uwanja wa Taifa.
Niang aliyedumu uwanjani kwa dakika
45 tu za kwanza, mashabiki wa Simba
walipata tukio moja tu la kuhadithia
juu ya nyota huyo katika sekunde 36,
alipopiga krosi iliyomgonga mkononi
beki wa Mwadui, Joram Mgeveke na
mwamuzi kuamuru penalti.
Hata hivyo, wachezaji wa Mwadui
walimzonga mwamuzi ambaye
baadaye alikwenda kumuuliza msaidizi
wake na kuamua mpira huo utolewe
nje ya eneo la penalti, adhabu ambayo
haikuzaa matunda.
Niang, ambaye ni mdogo wa
mshambuliaji wa kimataifa wa zamani
wa Senegal, Mamadou Niang
alionekana bado hajawa katika
kiwango chake na kushindwa
kushirikiana vizuri na Mussa Mgosi
kabla ya kutolewa wakati wa
mapumziko na nafasi yake kuchuliwa
na Hamis Kiiza.
Katika kile kinachooneka Simba bado
inasaka wachezaji wa kuimarisha
kikosi chake, leo watampokea
mshambuliaji N’Daw mwenye miaka
21, kutoka Senegal.
N’Daw alikuwa akichezea katika klabu
ya Dinamo Bucuresti ya Romania kabla
ya kuvunja mkataba wake kutokana
na kushindwa kutimiziwa masharti
yake ya kimkataba kwa mujibu wa
wakala wake, Paul Michel wa kampuni
ya Siavuma Sports ya Afrika Kusini.
Paul alilimbia gazeti hili jana kuwa
N’Daw alikuwa na wakati mgumu
Dinamo na kuamua kurejea nyumbani,
Senegal ambako alijiunga na klabu ya
Niarry Tally aliyoifungia mabao saba
katika ligi ya nchi hiyo.
Paul, ambaye ni wakala wa kocha wa
Simba, Dylan Kerr alisema N’Daw
atamaliza tatizo la ufungaji la klabu
hiyo pamoja na kuonyesha kiwango
cha juu katika michezo ya ligi na
kimataifa.
“Ni mchezaji mzuri ambaye naamini
atamaliza tatizo lao la ufungaji,
tulikubaliana niwaletee mchezaji, ni
matumaini yangu watamsajili kwa
sababu ni mshambuliaji wa kiwango
cha juu,” alisema Paul.
Mmoja wa viongozi wa Simba alisema
N’Daw alitegemewa kufika nchini
mapema zaidi, lakini matatizo ya
kupata vibali vya kufanya kazi
yalimkwamisha.
“Tumesikia sifa zake, lakini tulitaka
kumuona akicheza, japokuwa umri
wake mdogo wa miaka 21,
unatushawishi kwamba atakuwa
msaada kwetu kwa muda mrefu,”
alisema kiongozi huyo.
Tegete, Nizar warejea Taifa
Katika mchezo huo wa kirafiki ambao
makocha wa timu zote mbili walitumia
wachezaji wengi, lakini kuingia kwa
wachezaji wapya wa Mwadui, Jerryson
Tegete na Nizar Khalfan kuliamsha
shangwe kwa mashabiki wa Yanga
waliojitokeza uwanjani hapo.
Mwadui ilipata pigo dakika 77, baada
ya kipa wake Shabaan Kado kuumia na
kutolewa nje kwa machela na nafasi
yake kuchuliwa na Jackson
Abdulazack.
Pamoja na mabadiliko hayo, timu zote
zilionekana kushindwa kuwa na
mipango sahihi ya kutegeneza pasi za
mwisho za kupata mabao.
-

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni