other blog

Ijumaa, 21 Agosti 2015

NEC kutangaza matokeo uraisndani ya siku tatu

,



Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema itatangaza matokeo ya urais ndani ya siku tatu kwa sababu watatumia Mfumo wa Kusimamia Matokeo (RMS) ambao utawawezesha kupokea, kujumlisha na kutangaza matokeo.Licha ya kutakiwa kisheria kutangaza matokeo hayo ndani ya siku saba, NEC imebainisha kuwa mfumo huo utasaidia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa matokeo kutoka sehemu mbalimbali nchini na kuyatoa ndani ya siku hizo.Akizungumza na viongozi wa dini jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema maandalizi ya uchaguzi yanaendelea vizuri na muda wowote vifaa vya uchaguzi vitawasili nchini.Jaji Lubuva aliwataka viongoziwa dini kuwasukuma wauminiwao kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi na siyo kuwaelekeza mtu wa kumpigia kura.Alisema wao wana wajibu mkubwa katika kujenga umoja kwa sababu wanaaminiwa na wananchi.Alisema uandikishaji katika daftari la kudumu la wapigakura lilifanyika kwa mafanikio na NEC imeandikisha karibu watu milioni 24. Alisema kazi inayoendelea sasa ni uhakiki wa taarifa kwenye daftari hilo.“Jana (juzi) nilikuwa Angola kwenye mkutano, viongozi wenzangu walitupongeza kwa kuandikisha watu wengi kwa BVR ndani ya miezi mitatu licha ya kuwa na mashine chache,”alisema“Kenya waliandikisha watu milioni 14 kwa kutumia mashine 30,000 walizokuwa nazo, kwa hiyo tumefanya jambo kubwa, tunawataka nanyi viongozi wa dini muwahimize waumini kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi,” alisema mwenyekiti huyo.Uhakiki wa Daftari la WapigakuraJaji Lubuva alisema uhakiki wa daftari la wapigakura ulioanza Agosti 7, unalenga kutoa nafasi kwa wapigakura kuhakiki taarifa zao ili kuondoa kasoro mbalimbali zilizojitokeza wakati wa uandikishaji.Alikanusha taarifa zinazoihusisha tume hiyo na njama za kuficha taarifa za baadhi ya wapigakura.Alisema baadhi ya taarifa bado hazijaingia kwenye mfumo, kwa hiyo zile ambazohazijaonekana sasa zitaingia kwenye mfumo huo baada yasiku chache. “Wananchi wataweza kupata taarifa zilizoko kwenye database (rekodi) kwa kutumia simu zao kupitia ujumbe mfupi. Namba hiyo ni *152*00#,”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni